Na Gideon Gregory,Dodoma
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro amesema wataenda kuiendesha kibiashara ligi kuu ya Tanzania na hususani michezo ya Dabi ‘Derby’ za watani wa Jadi, Simba na Yanga ili kuhakikisha ligi hiyo inakuwa na thamani kubwa.
Waziri Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo leo Mei 23,2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024/25 na kuongeza kuwa watahakikisha timu zinatengeneza uchumi na zinafanikiwa kufika zaidi ya robo fainali katika mashindano ya kimataifa.
“Pia tutahakikisha tunaondoa migogoro kwa wadau wa utamaduni, sanaa na michezo kwa kuwa na katiba mfano kwa vyama na mashirikisho yote itakayotumiwa na vyama na mashirikisho yote ili kuboresha usimamizi katika utekelezaji wa majukumu kwa vyama na mashirikisho ya utamaduni, sanaa na michezo nchini”,amesema.