WIKI YA UTUMISHI: MASWALI YA MIKATABA, MIGOGORO YA ARDHI YATAWALA BANDA LA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Wakili wa Serikali, Catherine Paul amesema wengi wa Wananchi ambao wametembelea banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamekuwa wakitaka kuelimishwa kuhusu masuala ya Ardhi, Mirathi na mambo yahusuyo Mikataba.

Catherine ameyasema hayo hii leo Juni 23, 2025 wakati akielezea ufanisi wa kazi waliyoifanya na kutoa tathmonibya alichokiona katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yanayofanyika katika Viwanja wa Chinangali Park Jijini Dodoma, yaliyohitimishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema, “kwenye banda letu la Mwanasheria Mkuu wa Serikali tumetembelewa na watu 70, wengi wao wakitaka kujua kuhusu mambo ya Ardhi, Kirathi na yale yahusuyo mikataba, tumewaelimisha na wamefurahi kupata ufahamu.

Nao baadhi ya Wananchi waliotembelea banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiwemo Gift Daniel ambaye ni mkazi wa Dodoma, amesema wamefurahia wiki hiyo kwani wamejifunza mambo mengi ya kisheria.

Amesema, “tumeona mambo mengi lakini nimejifunza vitu vingi wakati nikiwa kwenye banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwahiyo siku ya leo imekuwa nzuri kwangu.”

Kwa upande wake Latifa Hamad amesema katika wiki hiyo ya Utumishi, ametembelea banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuwataka wazidi kuwaelimisha juu ya masuala ya kisheria.

“Nimepata fursa ya kuembelea mabanda mbalimbali, lakini nikiwa banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali nafurahi nimeuliza mwaswali na nimejibiwa nisiyoyajua nimeyajua na nimejibiwa kiufasaha.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *