Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wiki moja kabla ya kuanza mwezi mtukufu  wa ramadhani, hakuna dalili ya kusitishwa vita huko gaza

Siku tatu za mazungumzo kati ya Israel na kundi la Hamas kuhusu usitishaji mapigano huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka yameshindwa kufikia mafanikio, maafisa wa Misri wamesema, ikiwa ni chini ya wiki moja kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Kiislamu wa Ramadhani.

Haya yanajiri wakati huu, miezi mitano tangu vita kwenye eneo hilo ianze, imeacha sehemu kubwa ya Gaza kuwa magofu na kusababisha maafa makubwa ya kibinadamu, huku watu wengi, haswa katika eneo la kaskazini, wakihangaika kutafuta chakula.

Mashirika ya misaada yamesema imekuwa shida kupeleka vifaa na mahitaji mengine katika sehemu kubwa ya Gaza kwa sababu ya ugumu wa kuratibu na jeshi la Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *