Whozu na wenzake watakiwa kulipa faini

Kikao cha kusikiliza rufaa ya Wanamuziki wa bongofleva nchini @whozu_ @_bilnass_official na @mbosso_ kimefikia maamuzi ya kuwataka wasanii hao kulipa faini ili waweze kuruhusiwa kufanya kazi za sanaa nchini kwa kufuata maadili ya Kitanzania.

Maamuzi hayo yamefikiwa kwenye kikao chini ya uongozi wa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro kilichofanyika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam ambapo Mwanamuziki @whozu_ anatakiwa kulipa faini ya Milioni 5, @_bilnass_official Milioni Moja huku @mbosso_ akitakiwa kulipa milioni Tatu na wote kwa pamoja wameondolewa adhabu za kufungiwa ila wanatakiwa kulipa kwanza kisha waendelee na kazi zao.



Aidha msanii Whozu amepewa masaa sita ili kutekeleza azimio la kushusha wimbo huo kwenye “digital platforms” zote kama makubaliano yanavyoelekeza.


Mhe. Waziri amewahasa wasanii hao na wengine nchini kutumia ubunifu kwa kufuata taratibu ulioainishwa katika mwongozo wa uzingatiaji maadili katika kazi za sanaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *