Msanii wa muziki wa Kizazi kipya, Whozu ametangaza kuachana na lebo ya muziki aliyokua akifanyia kazi wakati anatoka kimuziki mpaka sasa, Whozzu kupitia taarifa rasmi amesema kwa sasa ni muda wake wa kujitafutia na kutengeneza wakina Whozu wengine.
Whozzu ameandika ‘Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa uweza na pumzi zake maana mpaka utakapopata wasada wa kusoma taarifa hii ni Ushahidi wa uweza wa Mungu kukuweka hai. Katika Maisha ya ukuaji wa kiumbe chochote binada-mu akiwemo huanza a tungaji wa mimba, kisha kuzaliwa,kutambaa, kutembea, kukimbia na kufikia hatua ya kujitambua na kuwaacha wazazi na Kwenda kujitegemea’ – Whozu.
‘Kiafrika kuna umri ukifika utalazimika au utafukuzwa kulala kwenye chumba cha wazazi ili waachie faragha yao na wenzio wapatikane. Nilipoingia kwenye tasnia ya Muziki nilipokelewa na kutunzwa vyema chini ya kaka zangu wamiliki wa TOO MUCH MONEY, walifanya kazi kubwa sana ya kuhaki-kisha kuwa nakuwa Whozu ambaye natambulika na nafanya makubwa kwenye tasnia ya muziki, kama ilivyo hatua za ukuaji imefika wakati sasa wa kutoka na kutolala tena kwenye chumba cha wazazi ili nitoe nafasi kwa wasanii wengine kutengenezwa na TOO MUCH MONEY na vile vile mimi nisi-mame ili nami nije kutengeneza kina Whozu wengine’. – Whozu
‘TOO MUCH MONEY kwang itabaki kuwa familia ya kudumu na nitashirikiana nao nyakati zote ushirikiano utakapohitajika. Hivyo kwa maneno haya machache namaanisha kuwa kwa sasa WHOZU hayupo tena chini ya TOO MUCH MONEY. Asanteni TOO MUCH MONEY kwa kuniamini na kuniaminisha kwa watanzania, sisi ni familia’ – Whozu.