Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

WHO Yalizwa na Dunia Kuuweka Kando Mgogoro wa Sudan

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dunaini, (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amelalamika vikali kutokana na dunia kutojali tena mzozo unaoendelea Sudan alipokua anatembelea nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, amewambia waandishi habari siku ya Jumapili alipotembelea mji wa Port Said, makao makuu ya muda ya serikali, kwamba kiwango cha mzozo ni cha kushtusha na kwamba hatua za kudhibiti ugomvi na kupunguza maafa miongoni mwa raia hazitoshi.

Tedros amesema kulingana na takwimu zilizopo, mgogoro wa Sudan hadi  sasa umesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 20, na watu milioni 10 wamelazimika kuyakimbia makazi yao na kuwa wakimbizi wa ndani  huku milioni 2 wakilazimika kukimbilia nchi za jirani.

“Huu ni mzozo mkubwa wa watu kupoteza makazi yao kwa wakati huu dunaini. na kiwango cha hali ya dhadura ni cha kutisha, na hakuna hatua za kutosha zinazochukuliwa kuzuia vita,” amesema mkuu huyo wa WHO.

Tedros ametoa wito wa kusitishwa mara moja vita na kufikia makubaliano yatakayopelekea suluhisho la kudumu la kisiasa na anatoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kuamka na kuisaidia Sudan.

Aidha amewatembelea wagonjwa katika hospitali moja huko Port Said na kukutana na maafisa wa serikali alipokua ananza ziara ya siku mbili katika mji huo unaoshikiliwa na serikali baada ya kufukuzwa Khartoum na kikosi cha dharura cha Sudan RSF.

Kulingana na mashahidi walozungumza na shirika la habari la AFP, mamia ya watu walikimbilia vitongoji vya kaskazini mwa Khartoum Jumamosi kufuatia mapigano makali kati ya jeshi na kikosi cha dharura karibu na kambi muhimu ya kijeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *