Ile kauli ya mpenzi wako ajaye humjui ni kweli wanetu! Hivi unajua wakati kundi la P Square wanatoa ‘Bizzy Body” mpenzi wa Paul Okoye (41), aka Rude Boy , Ivy Ifeoma (23) alikuwa na umri wa miaka mitano ambapo ni sawa na kuanza chekechea tu.
Mrembo huyo amethibitisha kupitia ukurasa wake Tiktok akicheza wimbo huo wa ‘Bizzy Body’ ambapo shabiki akamuuliza unacheza wimbo huo hivi wakati unataka ulikuwa na miaka mingapi? Ndio Bibiye akajibu nilikuwa na miaka mitano.
Wimbo huo umetoka 2005 na ulikuwa unapatikana kwenye albamu ya Get Squared