Mtangazaji nguli wa TV kutoka nchini Marekani, Wendy Williams, mnamo mwaka jana aligundulika kuwa na aphasia inayoendelea ambapo imesababisha kuwa na matatizo ya ubongo ya frontotemporal (FTD).
Taarifa za mwanamama huyo ambaye ifikapio Julai anatimiza miaka 60, zimetolewa siku ya jana na timu yake kupitia jarida la People Magazine, ambapo walisema yupo hai ila imebidi watoe taarifa kwa sasa baada ya uvumi usio sahihi kuenea juu ya afya yake.
Bi Williams, amefanya kipindi cha Wendy Williams Show kwa zaidi ya muongo mmoja yani alianza kipindi hicho mnamo 2008 mpaka 2021, ambapo afya yake ilianza kuleta shinda ila kiliisha mwaka 2022 huku kukiwa na shida za kiafya ambazo amekuwa akizikabili.