WC2O26: KILICHOWAPONZA STARS CHATAJWA

Kiza kimetanda kwa Taifa la Tanzania baada ya Taifa Stars kushindwa kufurukuta mchezo wa kufuzu kombe la Dunia la FIFA 2026 (WC2026), uliowakutanisha na Timu ya Taifa ya Zambia Chopolopolo.

Stars ilikubali kupokea kipigo cha 1-0 ikiwa nyumbani, kwenye mchezo wake wa mwisho wa Kundi E, huku Zambia ikiweka hai matumaini ya kufuzu kufuatia ushindi huo.

Mara baada ya mchezo huo, mashabiki wamekuwa na maoni tofauti wakisema benchi la ufundi pamoja na Kocha wanapaswa kujitafakari kwani kuna makosa ya wazi yanayojitokeza ikiwemo uchaguzi wa wachezaji na upangaji wa timu.

Wanasema Stars imekosa muunganiko na kwamba huenda kuna chuki binafsi, makosa yanayojurudia katika mbinu za ushindi na masuala ya Usimba na Uyanga ambayo mara zote umekuwa ukiathiri matokeo.

Zambia ambayo itacheza na Niger mchezo wa raundi ya mwisho ina matumaini ya kumaliza nafasi ya pili endapo itaibuka na ushindi ambao utakaoifanya kufikisha alama 15 nyuma ya Morocco yenye alama 21.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *