Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amewaongoza Maelfu ya Wananchi kufatilia hotuba ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Kijijini kwake Nandagala Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Sehemu ya salaam zake kwa wananchi waliojitokeza, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba Wananchi kuendelea kumuunga mkono Mh Rais kwenye uongozi wake na zaidi kwenye suala la nishati safi ya kupikia ambayo Rais Samia amekua balozi wa Dunia.