
WAZIRI MKUU wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa leo Machi 31, 2025 amejumuika na waumini mbalimbali wa dini ya Kiislam katika Swala ya Eid iliyofanyika kiwilaya kwenye Mtaa wa Maghalani, Ruangwa Mkoani Lindi.

Akizungumza baada ya swala hiyo, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa waumini mbalimbali na Watanzania kwa ujumla kuliombea Taifa, Viongozi wake pamoja na kudumisha amani, umoja na mshikamano tulionao nchini.

Swala hiyo ilihudhuriwa pia na Viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa mhe. Hassan Ngoma, Viongozi na waumini wa dini ya Kiislam.
