WAZIRI MKUU KUONGOZA HARAMBEE YA MEI MOSI KITAIFA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa usiku wa leo Aprili 5, 2025 anaongoza harambee ya kuwezesha maadhimisho ya Mei Mosi Kitaifa kwenye ukumbi wa Royal Village jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo yatafanyika Kitaifa mkoani Singida Mei 01, 2025 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete, Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamuhokya, Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Martha Mlata ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria harambee hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *