WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS SAMIA EXPO 2025 OSAKA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 22, 2025 ameondoka nchini kwenda Japan
kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maonesho ya World
Expo 2025 Osaka.

Taarifa iliyotolewa hii leo na Ofisi ya Waziri Mkuu, imeeleza kuwa Majaliwa pia atashiriki katika kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii ambalo litahusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan.

“Pia, Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Maonesho hayo yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajia kumalizika Oktoba 13, 2025,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho haya ya kimataifa,
ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *