Serikali imesema msimamo wake umebaki vilevile kuwa michango holela kwenye shule hairuhusiwi. Kauli hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akijibu maswali ya Wabunge katika kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu.
Amesema Kamati za shule zimeundwa kwa shule za msingi na Bodi za shule kwa shule za sekondari ambapo wajumbe wa bodi na kamati wanapatikana katika maeneo hayo hivyo wanapaswa kusimamia maendeleo na kushauri mwenendo wa shule hizo.
Aidha, Waziri Mkuu amesema ipo michango ambayo hakuna haja ya kuisubiri Serikali hivyo jamii inaweza kuweka mpango mkakati wa kuikusanya akitoa mfano wa choo cha shule kupata hitilafu jamii inaweza kuweka mkakati wa kuchangisha fedha ili ukarabati ufanyike.