Waziri Mkuu Wa Ethiopia, Abiy Ahmed, Amekanusha Taarifa Zilizotolewa Na Baadhi Ya Mashirika Yakidai Watu Wanakufa Kwa Njaa Katika Taifa Hilo La Pembe Ya Afrika Ambalo Linakabiliwa Na Mgogoro Mkubwa Wa Chakula Unaosababishwa Na Mizozo Ya Ndani Na Majanga Ya Hali Ya Hewa.

Ahmed Ametoa Maelezo Hayo Kwa Wabunge Baada Ya Kutolewa Tahadhari Kwamba Idadi Ya Watu Ambao Wanakabiliwa Na Uhaba Wa Chakula Inaweza Kufikia Milioni 11 Baadaye Mwaka Huu Katika Nchi Hiyo Ambayo Ni Ya Pili Kwa Idadi Kubwa Ya Watu Barani Afrika.