Waziri Makamba akanusha uwepo wa noti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhw. @jmakamba amekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya Habari Nchini zikidai kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imetambulisha noti mpya itakayotumika na Nchi Wanachama iitwayo SHEAFRA.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter (x) Mkamaba ameandika “Hizi taarifa si za kweli. Taratibu na vigezo vya kiuchumi na kitaasisi vya kufikiwa kwa Umoja wa Fedha (Monetary Union)/Sarafu Moja (Single Currency) kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki bado kukamilika. Mapendekezo ni kufika hatua hiyo mwaka 2031. Ukurasa rasmi wa Jumuiya ni @jumuiya.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *