WAZIRI KOMBO AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA JICA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Ando Naoki pembezoni mwa Mkutano wa Tisa wa TICAD uliofanyika jijini Yokohama.

Waziri Kombo amepongeza ushirikiano wa Tanzania na Japan kupitia JICA katika ufadhili wa uendelezaji wa sekta za kilimo; nishati; usafirishaji; afya; maji na uendelezaji wa rasilimali watu.

Katika kikao hicho walikubaliana kuendeleza ushirikiano huo hususan katika sekta za miundombinu bora, uendelezaji wa rasilimali watu; uchumi wa buluu na kilimo, hususan teknolojia ya kuongeza thamani malighafi za mazao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *