Waziri Bashungwa awasili Shinyanga, kukagua maafa ya EL-Nino

Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) amewasili Mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi ambapo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 8 Desemba 2023.

Katika ziara hii Waziri Bashungwa atakagua miundombinu ya barabara zilizoharibiwa na mvua kubwa za El-nino zinazoendelea kunyesha katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na Kahama Manispaaa.

Miundombinu hii iliyoharibiwa na mvua ni pamoja na barabara ya Shinyanga – Old Shinyanga, barabara ya Old Shinyanga – Solwa, barabara ya Solwa – Kahama na miundombinu mingine ya barabara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *