WAZAZI WATAKIWA KUTOWATEKELEKEZA WATOTO WENYE ULEMAVU KIPINDI CHA LIKIZO

Na Saulo Stephen – Singida.

Wazazi na Walezi wenye watoto wanaoishi na ulemavu wa aina mbalimbali wanaosoma katika shule ya msingi Ikungi Mchanganyiko,iliyopo wilayani Ikungi Mkoani Singida wametakiwa kuacha tabia ya kuwatelekeza wanafunzi hao shuleni hususani katika kipindi cha likizo na kuacha jukumu kwa walimu katika kusimamia malezi ya watoto hao.

Jambo fm imefika katika shule ya msingi Ikungi Mchanganyiko na kushuhudia baadhi ya watoto wenye ulemavu, wakiwa bado wapo shuleni licha ya kwamba ni kipindi cha likizo kwa wanafunzi hali iliyopekea kumtafuta afisa ustawi wa jamii wilaya ya ikungi, Roby Mhochi ambaye amekiriki kuwepo kwa changamoto hiyo huku akiwataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwatelekeza shuleni watoto wenye ulemavu kwani watoto hao nao wanahaki ya kupata malezi sitahiki kutoka kwa wazazi.

Hata hivyo kwa upande baadhi ya Wazazi na walezi wamezungumzia tabia hii ya baadhi ya wawazi na walezi ya kuwatelekeza shuleni watoto wenye ulemavu hususani kipindi hiki cha likizo wakisema kufanya hivyo si busara huku wakishauri wazazi wa namna hiyo kupata elimu na kuwa na uchungu dhidi ya watoto hao ambao nao wanahitaji faraja kutoka kwa wazazi,walezi pamoja na Jamii kwa ujumla.

Licha ya kwamba wanapitia changamoto mbalimbali kutokana na hali walionayo jambo hilo haliwazuii watoto wenye ulemavu kutoka shule ya msingi Ikungi mchanganyiko kuelezea matamanio ya kutimiza ndoto zao pindi watapofika umri wa utu uzima.

Naye Mwalimu Donald Bilal Adam kutoka katika shule hiyo ambaye ana changamoto ya kutoona amethibirisha uwepo wa changamoto zilizopo katika ufundishaji kwa wanafuzi wenye ulemavu na pamoja na kuyaomba mashirika mbalimbali pamoja na wadau kusudia upatikanaji wa nyenzo za ufundishaji kwa wanafunzi hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *