Wawili wauawa wakituhumiwa kuiba mpunga

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limeanza msako wa kuwatafuta wahalifu waliojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua watu wawili kwa kuwashambulia kwa mawe na silaha za jadi wakiwatuhumu kuiba gunia moja la mpunga.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema Leo Oktoba 31 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo Wilbroad Mtafungwa amesema kuwa tukio hilo limetokea Oktoba 30 Mwaka huu majira ya saa 11:30 jioni katika Kijiji na Kata ya Mwaniko wilayani Misungwi.

Inadaiwa Nkula na mwenzake Nzuri Kazungu walikuwa wamebeba mpunga kwenye pikipiki yenye namba za usajiri MC 989 CWU aina ya Kinglion iliyochomwa moto na kuteketea kabisa wakati wa tukio hilo wakitokea kijiji cha Budula-Ngudu wilayani Kwimba na walipofika Kijiji cha Mwaniko wilayani Misungwi ndipo walipozuiliwa na kuuawa na wahalifu hao .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *