WAWILI WANUSURIKA KUUWAWA KISA WIZI WA MITA ZA MAJI.

Watu wawili wamenusurika kuuwawa mtaa wa Masaki Kata ya Maalunga manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga baada ya kukutwa wakiiba dira za maji za mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (KUWASA).

Tukio hilo limetokea majira ya saa 9 usiku katika mtaa huo baada ya walinzi wanaolinda nyakati za usiku kuwaona waking’oa dira ya mteja na kuanza kuwapigia kelele kama anavyoelezea Kamanda wa sungusungu Joseph Mhangwa.

“Hili tukio limetokea majira ya saa tisa kuelekea saa kumi,Wezi hao walikuja kuiba mita kwa mteja mmoja ndipo walinzi wakawaona katika juhudi za kuwakamta wakakimbia wakaacha mfuko baada ya kuangalia tukakuta mita sita” Alisema Kamanda.

Kwa upande wake afisa Mahusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (KUWASA) amesema wizi wa dira bado upo hususan katika maeneo ya kata za Maalunga,Nyahanga na Mhongolo na kwamba kila mmoja aunganishe nguvu ili kuwabaini na kuwakamata watu hao.

“Wizi wa dira za maji bado upo husasn katika kata ya Nyahanga, Mhongolo na Malunga, Hivyo kazi ya ulinzi si ya sungusungu au polisi tushirikiane kwa pamoja nina hakika tunaweza kuzuia wizi huu” Amesema Mkama.

Naye mwenyekiti wa Mtaa Masaki Mugambi Samwel ametoa wito kwa wanachi kuweka doria za mara kwa mara ili kudumisha  ulinzi na amani katika mtaa huo.

“Nitoe rai kwa wananchi wa Mtaa wa Masaki tusilale kupitiliza hawa vibaka mida yao kuanzia saa nane usiku hadi alfajiri tukishiriana tunaweza kuwakamata na kuufanya mtaa wetu ukawa na amani” Amesema Mgambi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *