Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wawili wafariki kwa kula mboga ya uyoga

Watu wawili wamefariki dunia huku wengine 7 wakiendelea kupatiwa matibabu baada ya kula uyoga unaodhaniwa kuwa na sumu.
akizungumzia tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Wilbroad Mutafungwa amesema watu waliofariki ni Maua Mwilikwa (10) mkazi wa mabatini aliepoteza maisha katika hospitali ya Bugando huku mwingine akiwa ni Thomas Thomas (18) ambae alifariki dunia katika hospitali ya Sekou Ture.

Mutafungwa amesema watu hao ambao wanatoka katika familia mbili tofauti walifikishwa katika hospitali hizo mara baada ya kuanza kutapika na kuharisha hii ni kutokana na kula mboga aina ya uyoga ambayo inadhaniwa kuwa na sumu.

Mutafungwa pia amesema kupitia tukio hilo watu wengine saba walikula mboga hiyo na mara baada ya muda mfupi walianza kutapika kisha wakakimbizwa katika kituo cha polisi mabatini ila baada ya hali zao kutokua za kuridhisha watu hao walikimbizwa katika hospitali ya Sekou Ture ambapo wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zikiwa zinazidi kuimarika.

Aidha jeshi la polisi mkoa wa Mwanza linaendelea na jitihada za kumtafuta mtu aliewauzia uyoga huo ili aweze kuhojiwa huku pia jeshi hilo likiwaomba wananchi kuwa makini na vyakula wanavyokula ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *