WAWILI WA UWT KUWAKILISHA VITI MAALUM CCM KAGERA

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Mkoa Kagera (UWT) imefanya uchaguzi wa kuwapata wabunge wa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa Kagera wa nafasi za ubunge Viti maalumu na kufanikiwa kupata wagombea wawili wa viti maalum.

Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi na Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa, Yasmin Bachu alisema jumla ya wapiga kura walikuwa 1,483, ambapo kura moja iliharibika na hivyo kura halali zilikuwa 1,482.

Amesema, kwa mujibu wa matokeo hayo, Devotha Daniel alipata kura 1,308 na Samira Khalfani alipata kura 1,250 huku wagombea wengine 6 wagiwana kura zilizobaki.

Bi Yasmin Bachu amesema kuwa kwa mujibu wa taratibu za chama walioongoza kwa kura ndiyo walipita na kwasasa watasubiri kura za wabunge wanaogombea majimbo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Devotha Daniel na Samira Amour wameibuka washindi katika uchaguzi wa kura za maoni wa nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), kati ya wagombea wanane waliowania nafasi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *