Watumishi Wapya 46,000 Kuajiriwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Mhe. George Simbachawene amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan jana ametoa kibali cha kuajiri watumishi wapya 46,000 ambapo katika kibali hicho idadi ya walimu ni 12,000 huku ajira za afya zikiwa ni zaidi ya 10,000.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo leo Aprili 17,2024 bungeni Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa juu ya swali lililoulizwa na mbunge wa Viti Maalum Mhe. Benardeta Mushashu aliyetaka kujua ni lini Serikali itaajiri Walimu wa kutosha wa somo la hisabati na sayansi ili kuliokoa Taifa kutkosa wanasayansi siku zijazo.

Wakati huo huo, naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Zainab Katimba Serikali itaendelea kuajiri walimu wa masomo ya hisabati na sayansi na masomo mengine kadri ya upatikanaji wa fedha na uwezo wa kulipa mishahara. 

Mhe. Katimba ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum Mhe. Benardeta Mushashu aliyetaka kujua ni lini Serikali itaajiri walimu wa kutosha wa somo la hisabati na sayansi.

Aidha ameongeza kuwa Serikali inatambua upungufu wa walimu unaoukumba Mkoa wa Kagera hivyo imeandaa mkakati ambao utaweza kupunguza uhaba huo.

 Kwa upande wake Naibu Spika Mussa Azzan Zungu ameitaka serikali wakati wa utoaji wa ajira hizo kutoa kipaumbele kwa walimu ambao wamekuwa wamekuwa wakijitolea kwa kipindi kirefu kabla ya kuwachukua wengine wapya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *