WATUMISHI WA UMMA WAKUMBUSHWA KUWATUMIKIA WANANCHI IPASAVYO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan
amewakumbusha Watumishi wa umma kote nchini kuwa wamekasimiwa majukumu ya kuwatumikia lWananchi na amewataka wasimame ipasavyo katika nafasi zao na kutimiza majukumu yao.

Rais Dkt. Samia ametoa msisitizo huo hii leo Februari 25, 2025 wakati akizungumza na Wananchi na Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni mara baada ya kufungua rasmi Jengo la Halmashauri hiyo.

Aidha, Rais Dkt. Samia ameeleza imani yake kuwa jengo hilo linaimarisha utawala bora na huduma kwa Wananchi ambapo Jengo hilo ni moja kati ya majengo 122 yaliyojengwa katika
Halmashauri mbalimbali nchini tangu mwaka 2021 ikiwemo jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli ambalo Rais Dkt. Samia amelizindua jana tarehe 24 Februari, 2025.

Awali akiwa Wilaya ya Handeni, Rais Dkt. Samia ameweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Miji 28 unaoenda kuimarisha upatikanaji wa maji katika Wilaya za Handeni, Korogwe, Muheza na Pangani.

Katika hatua nyingine, akiwa Wilaya ya Kilindi, Rais Dkt. Samia ametambua mchango uliotolewa na marehemu Beatrice Shelukindo wakati wa uhai wake katika kutetea haki za wanawake na kupitia nafasi za uongozi alizozishika ikiwemo Ubunge wa Jimbo la
Kilindi na Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa heshima yake, Rais Dkt. Samia
ameelekeza Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Tanga ipewe jina la Beatrice Shelukindo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *