WATUMISHI WA UMMA EPUKENI RUSHWA WANANCHI WAPATE MAENDELEO – DKT. FATUMA

Na Saulo Stephen – Singida.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga amewataka Watumishi Mkoani humo kuepuka vitendo vya rushwa, ili waweze kufikia malengo sahihi ya kuwaletea maendeleo Wananchi.

Dkt. Fatuma ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo maalum kwa Watumishi wa Umma Mkoani Singida, kuhusu masuala ya Rushwa mahali pakazi .

Amesema, vitendo vya Rushwa vikifanywa na watumishi wa umma inakuwa ni fedheha na aibu kwa Jamii na kuondoa imani kwa wananchi ambao wanawaamini katika kuwaletea maendeleo kwani wananchi wanawaangalia watumishi wa umma kama mfano na kioo katika jamii.

Kwa upande wake Afisa kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Onesmo Mdegela amesema vitendo vya Rushwa vinasababishwa na mmomonyoko wa maadili na hivyo watumishi wa umma wanatakiwa kufata kanuni na miongozo ya kazi ili waweze kuepukana na vitendo vya Rushwa ili waweze kuwatumika wananchi kwa haki na usawa.

Aidha. alitumia nafasi hiyo kuelezea majukumu ambayo yanafanywa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU kama vile kufatilia Miradi ya Maendeleo ,Kutoa elimu kuhusiana na Maswala ya Rushwa kwa makundi mbalimbali katika Jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *