Na Saada Almasi – Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga amewataka watumishi katika halmashauri ya Bariadi vijijini kuendelea kufanya kazi kwa upendo na uadilifu ili waweze kuleta maendeleo yaliyokusudiwa na serikali kwa wananchi wake.
Akiwa katika kuhitimisha baraza la mwisho la madiwani kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Simiyu,Simalenga amesema kuwa ni nadra sana kukutana na watumishi wanaochapa kazi kwa uaminifu mkubwa isipokuwa sehemu ambayo kuna misingi mizuri ya uongozi na karama ya utii kama ilivyo katika halmashauri hiyo.

“baraza hili ni miongoni mwa mabaraza yenye utii na uadilifu uliopitiliza na hii ni kutokana na misingi ya uongozi mliyonayo mmejengeka katika kuzungumza lugha moja na niseme tu kwamba Rais wa nchi alipokuwa ziarani mkoani hapa ameridhishwa na mapokezi na maandalizi yenu mazuri,” amesema DC Simalenga.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa baraza hilo umeleta matokeo chanya hasa katika sekta ya elimu ya sekondari kwa kuufanya mkoa kushika nafasi ya tano kitaifa ambapo halmashauri hiyo ikitoa shule hiyo huku kitaifa ikiwa miongoni wa wilaya zilizo katika kumi bora na kusema kuwa ushirikiano uliopo kati ya mwenyekiti wa halmashauri,kaimu mkurugenzi na kila mtu aliye katika halmashauri hiyo.

Naye mwenyekiti wa halmashauti hiyo Mayalla Lucas amewashukuru madiwani wa baraza hilo ushirikiano mzuri waliouonyesha katika uongozi wake uliofanya halmashauri hiyo kushika nzuri kitaifa huku akieleza baadhi ya miradi ya kimaendeleo iliyotekeleza ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya.
“Yapo mengi tuliyoyafanya katika kipindi cha miaka mitano ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za sekondari 8 zahanati mpya 11 na zinatoa huduma,vituo vya afya viwili,tumepeta gari la wagonjwa,shule za msingi 15 watoto wanasoma na mengine mengi kama umeme na maji ,maendeleo ambayo yasinge wezekana kama tusingekuwa na ushirikiano mzuri”amesema Mayalla.

Aidha, Mayalla ameongeza kuwa maendeleo yaliyofanyika wilayani humo ni jambo la kujivunia kwani zipo baadhi ya halmashauri zilizopokea pesa za serikali kama halmashauri hiyo lakini hadi sasa hakuna utekelazaji wala kukamilika kwake
Mabaraza ya Madiwani ya Halmashauri zote nchini yamefungwa rasmi kufuatia agizo la Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania likifuatiwa na maelekezo ya waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) za kuhitimisha mabaraza hayo kwa kupokea na kujadili ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) na kuzijadili ambapo halmashauri hiyo imepokea hati safi.
One response to “WATUMISHI BARIADI ENDELEENI KUFANYA KAZI KWA UPENDO NA UADILIFU – DC SIMALENGA”
HONGERENI. SANA WAHESHIMIWA MADIWANI WETU WA HALMASHAURI YA BARIADI KWA KAZI KUBWA MLIOFANYA YA KULETA MAENDELEO NA KUIJENGA HALMASHAURI ,MKIONGOZWA NA JEMEDARI WETU MKUU WA WILAYA SIMON SIMALENGA•
MWENYEZI MUNGU AWABARIKI SANA ,NA KUWAONGOZA
ILI25/ OCT /2025 MURUDI TENA