Watumishi 11 wa Manispaa ya Kigoma Ujiji pamoja na TAMISEMI wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu uchumi namba 3 ya mwaka 2023 yenye mashtaka 11 likiwemo la utakatishaji fedha Sh.milioni 463.5.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2023/11/8804c538-ae9b-4b02-9a1d-f163b7366d03-jpeg.webp)
Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Hassan Momba, Wakili Mwandamizi wa Serikali Anosisye Erasto ameieleza mahakama kuwa washitakiwa walitenda makosa hayo kati ya Juni 1, 2022 na Juni 5 2023 katika Manispaa ya Kigoma ujiji na Jiji la Dodoma
Washitakiwa katika kesi hiyo ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ujiji Athumani Msabila, watumishi wa ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dodoma Aidan Mponzi na Tumsifu Kachira.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2023/11/6e476dea-e0a7-426a-ae53-76e6714666fa-jpeg.webp)
Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza mashauri yao ikiwemo shtaka la uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara.
Kesi hiyo imehairishwa hadi Novemba 20 mwaka huu itakapotatajwa tena kwa ajili ya kutoa uamuzi wa dhamana kwa washitakiwa watano ambao hawahusiki na shitaka la utakatishaji fedha kama watakuwa na haki ya kupata dhamana.