WATUHUMIWA WA MAUAJI YA MTOTO GRAISON WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MARA YA KWANZA…

Watuhumiwa wawili wa kesi ya mauaji ya Mtoto Grayson Kanyenye (6) mtoto wa mfanyabiashara Zaitun Shaban maafuru ‘JOJO’ wamefikishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi jijini Dodoma.

Watuhumiwa hao wakazi wa Ipagala jijini Dodoma Kelvin Joshua (27) na Tumaini Msangi (28) ambaye ni bondiawaliffikishwa mahakamani hapo mbele ya hakimu mkazi Denis Mpelembwa Disemba 30,2024 na kusomewa shitaka hilo kwa Mara ya kwanza.

Kesi hiyo namba 35951/2024 imesomwa mbele ya hakimu mkazi Denis Mpelembwe na wakili wa serikali Patricia Mkina ambaye amesema kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo kwa kukusudia mnamo Disemba 25 Mwaka 2024 katika eneo la ilazo Jijini Dodoma.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 13,2025 na watuhumiwa wamerudishwa mahabusu kwasababu kesi hiyo haina dhamana kwa mujibu wa hakimu Denis Mpelembwe anayesimamia kesi hiyo.

Ikumbukwe kuwa Grayson Kanyenye (6) aliuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani usiku wa kuamkia Disemba 25,2024 katika eneo la Ilazo jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *