Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa saba wanaotuhumiwa kumteka na kumtishia kwa Silaha ,Honey Noah (29) mkazi wa Masaki jijini Dar es salaam, ambaye walimteka akiwa ndani ya gari lake aina ya Rav 4 na kumshikilia kwa nguvu kwa kipindi cha siku nne wakidai kiasi cha Dola milioni 3.5 kwa baba yake
Akiongea na waandishi wa habari Kamanda Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro anasema kutokana na chunguzi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao mmoja wapo ni raia wa Canada mwenye asili ya Kisomalia, na watuhumiwa wote leo watafikishwa Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazowakabili za kumteka, kumtishia kwa silaha, kumshikilia kwa nguvu na kudai pesa kwa nguvu .