Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limeendelea kufanya misako na operation mbalimbali kwa lengo la kuzuia na kudhibiti vitendo vya uhalifu sambamba na kuwakamata wahalifu pamoja na vielelezo vinavyohusiana na makossa mbalimbali.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake hii leo Agosti 27, 2026, Kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP. Janeth Magomi amesema wamewakamata Watuhumiwa 153 kwa makossa mbalimbali,pamoja na wahamiaji haramu 47 ambao wamekamatwa katika mameneo tofauti ya mkoa wa Shinyanga kwa kuingia nchini bila kuwa na vibali halali.
Amesema, katika operatio hizo jeshi hilo pia limeafnikiwa kukamata vielelezo kadhaa ambavyo ni pamoja na noti bandia zenye thamani ya shilingi 1,530,000, mirungi kilogram 43,bangi yenye uzito wa kilogram 380,pikipiki 26,mifuko 13 ya saruji ,nondo 20,mbao 70 ambapo 59 kati ya hizo zina urefu wa futi 8 kila moja ,baiskeli 1 na mtungi mmoja wa kuzimia moto.

Kwa upande wa mafanikio wa mafanikio ya kesi mahakamani kamanda Magomi amesema jumla ya washitakiwa 24 wamepatikana na hatia na kuhukumiwa vifungo vya kuanzia miezi 4 hadi miaka 30 kwa makossa mbalimbali ikiwemo wizi,kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu,ubakaji unyanyasaji pamoja na makosa mengine.
Katika kuimarisha usalama barabarani mkoani humo,jeshi hilo limeendesha operatio mbalimbali zilizowezesha kubaini jumla ya makossa 5291 ya ikiukwaji wa sharia za usalama barabarani,ambapo kati ya kosa hayo 4079 yalihusu magari huku 1212 yakihusu bajaji na pikipiki na kwamba wahusika wote wamechukuliwa hatua kwa mujibu wa sharia.
Amesema, katika kipidi cha miezi 3 jumla ya madereva 6 walifungiwa leseni zao za udereva baada ya kubainika kuwa wameendesha magari kwa mwendokasi wa kilomita 116 kwa saa,huku akitoa wito kwa madereva wote mkoani humo kufuata sharia za usalama barabarani, ili kuepusha ajali, kulinda maisha pamoja na mali za wananchi


