Watu watatu wakazi wa kijiji cha Mwasilimbi kata ya Ihusu Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo, kwa tuhuma za kukutwa na Wanyamapori aina ya swala 28 wakiwa wamewaua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Edith Swebe amasema kuwa watu hao walikamatwa katika operesheni ya pamoja kati ya Jeshi la Polisi na Jeshi la Uhifadhi.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Polisi ameeleza kuwa watuhumiwa pamoja na vielelezo watafikishwa mahakani kwa hatua za kisheria.