Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Watu sita wafariki Njombe

Watu 6 waliokuwa wakisafiri kutoka Makete kuelekea Tandala wilayani Makete mkoani Njombe wamefariki dunia baada ya basi (Hiace) walilokuwa wakisafiria kupinduka

Ajali hiyo imetokea Oktoba 13,2023 majira ya saa kumi na moja jioni katika kijiji cha Ndulamo ambapo kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe John Imori amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi aliokuwa nao dereva

Majeruhi 12 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Consolata Ikonda, ambapo mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Juma Mfanga amesema tayari serikali ya mkoa imeagiza madaktari kutoka hospitali ya rufaa mkoa wa Njombe waje kusaidiana na wa Ikonda kuwatibu Majeruhi

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka na viongozi wa mkoa na Wilaya, wa chama cha Mapinduzi na Serikali wamefika kuwajulia hali majeruhi na kutoa pole kwao na kwa familia za waliopoteza maisha na kusema serikali ya mkoa itakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha majeruhi wanatibiwa na kupona, na marehemu wanazikwa kwa heshima zote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *