Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Watu nane wafariki dunia na wengine 36 wajeruhiwa kwa ajali ya Basi mkoani Mwanza

Watu wanane wamefariki dunia na wengine 36 wamejeruhiwa mara baada ya basi la Abiria kampuni ya Nyehunge kugongana na basi la kampuni ya Asante Rabi ajali iliyotokea majira ya saa kumi na mbili asubuhi katika eneo la Ukiluguru wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza DCP Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema ajali hiyo imetokea baada ya basi la Asante Rabi lenye namba za usajili T 458 DYD lililokua likitoka mkoa wa Mwanza kwenda mkoa wa Arusha kugongana na Basi la kampuni ya Nyehunge lenye namba za usajili T 281 EFG linatoka mkoa wa Morogo kwenda mkoa wa Mwanza.

“Dereva wa basi kampuni ya Nyehunge alianza kuchepuka ‘overtaking’ magari yaliyokuwa mbele yake pasipo kuchukua tahadhari lakini pia eneo hili lina kona kali na kuna alama ambayo inamkataza kufanya hivyo,”amesema DCP Mutafungwa.
Baadhi ya mashuhuda wamesema ajali hiyo imetokea wakati dereva wa Basi la kampuni ya Asante Rabi akijaribu kulipita gari jingine ambapo wakati anafanya hivyo lilitokea gari la kampuni ya Nyehunge ndipo alipogongana na gari hilo.

Nae Mganga Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Clement Morabu amesema mpaka sasa wana jumla ya majeruhi 39 ambapo kati ya hao majeruhi 21 wamepelekwa katika kituo cha afya Usagara huku wengine 18 wakipelekwa katika hospitali ya wilaya na jumla ya watu nane wamefariki akiwemo mtoto wa miezi tisa.

“Tulipokea miili saba pamoja na mtoto mmoja mwenye umri wa miezi tisa ambaye alikuwa katika hali mbaya na alifariki dunia katika hospitali ya Wilaya. Kati ya miili hiyo wakike ni watatu na wanaume watano,” Dkt Morabu

Katika hatua nyingine Dk.Morabu amesema baada ya kupokea taarifa ya ajali hiyo walifika moja kwa moja katika eneo la tukio na kukuta majeruhi zaidi ya 50 na kufanya uchambuzi ambako majeruhi 21 waliokuwa kwenye hali ya kawaida walipelekwa katika Kituo cha Afya Usagara.

“Wengine 18 tukawapeleka katika Hospitali yetu ya Wilaya na majeruhi wote 39 wahudumiwa kwa usahihi na mpaka sasa kati yao majeruhi wanne ambao walikuwa katika hali mbaya zaidi wakihitaji vipimo kama CT-Scan tumewapa rufaa katika Hospitali ya Rufaa Kanda Bugando baada ya kuwa tumewapa huduma ya kwanza na majeruhi waliokuwa katika majeraha ya kawaida wote tumewahudumia na kuchukuliwa na ndugu zao,”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *