Watu Mil 17 hufariki kila mwaka kwa ugonjwa wa moyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk Peter Kisenge amesema Ugonjwa wa moyo unashika nafasi ya tatu katika magonjwa yanayochangia vifo vingi nchini huku takwimu zikionesha kuwa siku za mbeleni vifo vitaongezeka kutokana na tatizo hilo.

Dk Peter Kisenge amesema hayo leo Dar es Salaam katika siku ya kwanza ya kambi ya kupima wananchi magonjwa ya moyo pamoja na magonjwa yasiyo ya kuambukiza inayofanyika katika hospitali ya Dar Group Dar es Salaam.

Dk Kisenge amesema ukiacha na ugonjwa wa malaria na Ukimwi, wagonjwa wa moyo umekuwa wakiongezeka na duniani kote magonjwa ya moyo yanaongoza ambapo watu milioni 17 hufa kila mwaka kwa tatizo hilo.

Kuhusu huduma hiyo kwa mikoa mingine amesema tayari wameshazunguka katika mikoa zaidi ya 11 na kuwaona wagonjwa zaidi ya 7000 na kote walikopita ugonjwa wa Shinikizo la damu unaongoza kwa asilimia 25 na kuhimiza wananchi wakjitokeze kupima kutokana na mtindo wao wa maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *