Takwimu zilizotolewa leo na Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Profesa Paschal Rugajjo imesema jumla ya mikoa 17 nchini imekumbwa na ugonjwa wa macho mekundu ujulikanao kitaalamu kama viral keratoconjunctivitis (red eyes) na watu 5,359 wametajwa kuathirika.
Kufuatia kusambaa huko, wizara imewaasa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo unaosababishwa na maambukizi ya kirusi kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho.
Amesema hadi kufikia Ijumaa Januari 26, idadi ya waliofika kwenye vituo vya afya walifikia 5,359 kutoka wagonjwa 1,109 Januari 19.