Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa Jina la Boliva Betram Mapunda (26) Askari wa Kampuni ya Suma Guard Mkazi wa Kijiji cha Mteka Songea amefariki alipokuwa akipatiwa matibabu kwenye kituo cha afya mbambabay,Baada ya kuvamiwa kisha Kushambuliwa na wananchi waliokuwa na silaha kali za Jadi ikiwemo mapanga,Nyengo na mishale alipokuwa kwenye Lindo la hifadhi ya misitu ya Safu za Milima ya Livingstone iliyopo mpakani mwa Wilaya ya Nyasa na Mbinga.

Tukio limetokea Novemba 19,2023 majira ya saa mbili Asubuhi katika kijiji cha mkali kilichopo Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Akibainisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polsi mkoa wa Ruvuma ACP Marco Chilya amesema, chanzo cha tukio ni Wananchi wa Vijiji vya Namkuka na Mkwakwani wanadai kuwa maeneo hayo ya hifadhi yanayomilikiwa na Wakala wa Misitu TFS ni maeneno yao ambayo yalichukuliwa na Serikali bila wao kulipwa Fidia.
Aidha,kamanda Chilya amesema baada ya tukio hilo Watuhumiwa 40 waliokuwa wamejificha kwenye mapango ya Safu za milima ya Livingstone jirani na Vijiji vya Mkalia na Mkuwa wakiwa na silaha zao za jadi wamekamatwa. Kamanda Chilya amewaagiza wamiliki wa makapuni yote ya ulinzi mkoa wa Ruvuma kuhakikisha bunduki zao zinakuwa na risasi.
“Jeshi la Polisi litafanya ukaguzi kwenye malindo yao na na ikigundulika bunduki haina risasi tutachukua hatua kali kwa wamiliki wa Kampuni ya ulinzi husika.”