Wananchi Mkoani Tabora wamevamia kituo cha polisi Kitunda na kukiteketeza kwa moto kwa sababu ambazo mpaka sasa hazijafahamika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora , Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema kuwa hakuna madhara yaliyotekea kwa binadamu na kuwa mpaka sasa hawezi kutoa taarifa chanzo cha tukio hilo kwani yupo kwenye shughuli za mwenge ila hadi sasa washukiwa 28 wameshikiliwa kwa ajili ya mahojiano Zaidi.
.
“Nipo katika shughuli za Mwenge siwezi kutoa taarifa kamili kuhusu tukio hilo lakini hadi sasa tunawashikilia Watuhumiwa 28, wanaendelea kuhojiwa ili kujua chanzo cha kukichoma moto kituo, pia upelelezi unaendelea.”-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora , Richard Abwao.