Watu 15 wamekamatwa kwa tuhuma za wizi wa Marobota 12,500 ya kuhifadhia tumbaku(Majafafa) yenye thamani ya zaidi bilioni 1.4 za Kitanzania kufuatia operesheni inayoendeshwa na Serikali ya mkoa wa Tabora.
Taarifa ya kukamatwa kwao imetolewa na waziri wa kilimo Mh. Hussein Bashe akiwa mkoani Tabora wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa Katika operesheni hiyo wapo pia viongozi wa vyama vya ushirika mkoani Tabora ambao pia wanatuhumiwa kuwauzia wakulima magunia ya kuhifadhia Tumbaku huku wakijua kinyume cha sheria.
“Tumekuwa na operesheni maalumu ya kuwasaka watu wanaowauzia wakulima Majafafa ambapo kiutaratibu wa zao hili wakulima hawapaswi kuuziwa wala kuuza, katika operesheni hii tumekamata watu 15 waliyokuwa wameficha magunia haya kwa ajili ya kuwauzia wakulima katika msimu huu wa kilimo ambapo magunia zaidi ya elfu mbili Mia tano yenye gharama ya shilingi bilioni 1.4 tumeyakamata sheria itachukua mkondo wake watu hawa watawajibishwa kwasababu hii pia ni njia moja wapo ya kuhujumu wakulima na hii operesheni haitoishia hapa tutaendelea na kazi hii na itafanyika uchunguzi hata kwenye makampuni makubwa ya tumbaku ili hii mchezo wa wizi huu uishe katika Sekta ya tumbaku” – Waziri Bashe.