Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Watoto wawili wafariki kwa kukosa hewa ndani ya gari

Watoto wawili wanaokadiriwa kuwa na miaka kati ya 6 na 7 wamefariki dunia kwa kukosa hewa wakati wakicheza ndani ya gari katika Kitongoji cha Ng’ung’ula Kijiji cha Jomu kata ya Tinde Wilaya ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Jomu, Juma Warioba na Diwani wa kata ya Tinde, Japhar Kanolo wamesema tukio hilo limetokea Agosti 22, 2023 saa 12 jioni wakati watoto wakicheza ndani ya gari ambalo lilijifunga, wazazi wao bila kujua kinachoendelea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akidai wazazi wa watoto hao walitokea Mwanza kwenda kusalimia nyumbani kwao Tinde.

“Jeshi la polisi tumepokea taarifa hizi, wazazi walitoka Mwanza wakiwa na gari lao kwenda kusalimia nyumbani kwao Tinde, walipofika pale hawakufunga milango ya ile gari na vioo vilikuwa vimefungwa hivyo gari lilijifunga na watoto kukosa hewa,” ameeleza Magomi na kuongeza;

“Baada ya wazazi kushuka watoto walirudi kwenye lile gari wakaanza kuchezea likajifunga, kwa mujibu wa Daktari watoto wale walifariki kwa kukosa hewa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *