Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Watoto Wawili wa Familia Moja Wafariki Kwa Ugonjwa Usiojulikana

Mama Mlezi wa Watoto waliofariki Ester James akizungumzia namna tukio hilo lilivyotokea.

Watoto wawili wa familia Moja wakazi wa Mtaa wa Uwanja Kata ya Nyankumbu Halmashauri ya Mji Geita Mkoani Geita wamefariki dunia kwa ugonjwa usiojulikana huku mama yao mzazi na watoto wengine wawili wakilazwa katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Geita baada ya kuugua ghafla.

Tukio hilo limetokea April 19 mwaka huu Katika Mtaa huo ambapo Bibi wa watoto hao Juliana Pamoshi amesema walianza kutapika na kuhara mfululizo na baadae kuishiwa nguvu kwa nyakati tofauti huku akiwataja waliofariki dunia kuwa ni Kelvin Marco(11) na Monderic Marco(3).

Akithibitisha kutokea kwa vifo vya watoto hao wawili ambao wamefariki ghafla Mganga Mkuu katika hospitali ya Mji Geita Dkt.Sande Mwakyusa amesema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha vifo hivyo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Geita Hashimu Komba amekiri kutokea kwa vifo hivyo na kuagiza Jamii ya wilaya ya Geita kuchukua tahadhari kwa kutumia Maji safi na salama pamoja na kuagiza wakurugenzi wa halamsahauri zote mbili ikiwemo Mji pamoja na wilaya kutenga vikusanya taka katika maeneo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *