WATOTO WALIOJITEKA WAKITAKA PESA WAPATIKANA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limesema kuwa Januari 29, 2025, liliwapata na kuwahoji Wasichana wawili mmoja wa Miaka 16 Mwanafunzi wa Kidato cha Pili (16) na Mwanafunzi wa Darasa la saba (12), wote wakazi wa Vijibweni Kigamboni Dar es salaam, kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwa kutengeneza mazingira kuwa wametekwa na kwamba watekaji wanataka pesa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, ufutiliaji ulifanywa na kufanikiwa kubaini watoto hao walipokuwa na baada yamahojiano ya kina walikiri kutengeneza tukio hilo la uongo, ili waweze kujipatia pesa kwa udanganyifu toka kwa wazazi wao baada ya kutoweka Januari 26, 2025 na kuelekea Longoni Beach ambapo walikesha hapo hadi Januari 27, 2025 asubuhi na baadae kuelekea maeneo ya Tungi hadi walipokamatwa wakizunguka.

Jeshi hilo limesema linalaani vitendo hivyo vya watu vyenye lengo lakujipatia pesa kwa njia za udanganyifu huju likibainisha kuwa, katika kipindi cha Desemba hadi Januari 2025 baadhi ya watuhumiwa mbalimbali walipatikana na hatia ikiwa ni pamoja na Idrisa Rashid (35) Mkazi wa Kwembe, Kimara.

Mkazi huyo alihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kubaka kwenye Mahakama ya Wilaya Kinondoni, huku Paul Elisha (37) mkazi wa Mbezi Beach kwenye Mahakama hiyo hiyo ya Kinondoni akihukumiwa kifungo cha Maisha jela kwa kosa la kubaka na Jackson Mgeta (34) mkazi wa Kawe alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.

Aidha, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa Wananchi kuendelea kushirikiana ili kuimarishamifumo ya ulinzi shirikishi ikiwa ni pamoja na kutekeleza falsafa ya ulinzishirikishii ili kuzuia vitendo vya kihalifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *