Watoto wa kiume wapo hatarini ya kutopata malezi bora.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali inatambua kuwa mtoto wa kiume yupo katika hatari ya kutopata malezi bora, hivyo ipo katika mchakato wa kuandaa mpango wa malezi na makuzi ya watoto kwenye umri wa awali na mpango wa pili wa kuwawezesha na kuwaendeleza vijana balee kuanzia umri wa miaka 10 hadi 19.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo Bungeni, Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe ambaye amehoji mpango wa Serikali katika kulinda na kumjengea mtoto wa kiume uwezo.

Ameongeza kuwa hivi karibuni kumeibuka utamaduni wa kumtetetea mtoto wa kike lakini tunao utamaduni wetu ambao mtoto wa kiume ni baba au kiongozi wa familia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *