Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Watoto 752,877 kupewa kinga ya kichocho na minyoo

Jumla ya watoto 752,877 wenye umri wa miaka 5 hadi 14 kutoka katika kata 130 mkoani Shinyanga wanatarajiwa kupatiwa dawa za kingatiba ya minyoo ya tumbo na kichocho kupitia kampeni ya utoaji wa Kingatiba hiyo inayotarajiwa kufanyika Novemba 24 kwa mkoa mzima.

Akizungumza hii leo Novemba 17,2023 katika kikao cha kuweka mkakati wa kampeni hiyo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christine Mndeme amesema kwamba miongoni mwa watoto hao,watoto 286,782 watapata chanjo ya kichoho,466,095 wakitarajia kupatiwa chanjo ya minyoo ya tumbo na kutumia fursa hiyo kuelezea umuhimu wa kingatiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *