Watoa Mikopo Kaushadamu Wakamatwa Dodoma

Jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) limewakamata watu Wawili wanaoshukiwa kwa tuhuma za kukopesha fedha bila kufuata masharti na kupelekea watu wanaochukua mikopo hiyo kuchukuliwa vitu vyao vya thamani.

Hayo yameelezwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na hali ya uhalifu ndani ya mkoa huo na kuongeza kuwa washukiwa hao waliachiliwa kwa dhamana na upelelezi unaendelea ili waweze kupelekwa mahakamani.

“Msako utaendelea kwani wapo waliopewa vibari wanatoza riba kubwa na tunawasihi wafuate madharti ya kukopesha na ambao hawana vibali wavitafute,”amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *