WATATU WALIOFARIKI KWA AJALI KILIMANJARO WATAMBULIWA

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa, imeeleza kuwa watu watatu waliofariki katika ajali ya Gari dogo aina ya Rav4 lenye namba za usajili T. 592 EKU, lililogongana na basi hii leo Februari Mosi 2025, wametambuliwa.

Waliofariki ni Dereva Paul Donald Sita (25) mkazi wa Dar es Salaam, Exaud Elipokea Mbise (65) na Apaikunda Mathayo Ayo (61), wote wakazi wa Mkoa wa Arusha ambao kwa pamoja walikuwa katika gari hilo dogo wakitokea Dar es Salaam kuelekea Moshi

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari dogo kujaribu kuyapita magari mengine, bila kuchukua tahadhari na kugongana uso kwa uso na basi hilo la abiria aina ya Yutong lenye namba za usajili T. 612 EGV Kampuni ya Ester Luxury lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam.

Ajali hiyo, ilitokea eneo la Kanani, kata ya Kiborloni, tarafa ya Moshi Mashariki Wilaya yaMoshi Manispaa majira ya saa 12:40 asubuhi na Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya rufaa KCMC Moshi kwa uchunguzi nataratibu zingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *