WATATU WADAKWA WAKITOROSHA DHAHABU YA MILIONI 700

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikilia watu watatu waliokamatwa wakisafirisha dhahabu Gramu 3263.72 zenye thamani ya shilingi milioni 749,509,531.94 kinyume cha sheria.

Watuhumiwa hao walikamatwa Machi 24, 2025 saa 5 usiku huko Mtaa wa Kapera Wilayani Bukombe wakisafirisha mzigo huo kwa njia za magendo kwa kutumia gari aina ya Toyota Premio lenye namba za usajili T. 739 EEH mali ya Emanuel Kidenya.

Waliokamatwa ni Yohana Idama (34), Mkazi ya Nyamhongolo Wilayani Ilemela Mkoqni Mwanza, Moshi Manzili (26), Mkazi wa Bariadi MkoanibSimiyu na Hamidu Salum (25), Mkazi wa Nyasubi Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Polisi imeeleza kuwa uchunguzi wa tukio hili kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine unaendelea kufanyika ili kuwabaini na kuwakamata watakaobainika kujihusisha na uhalifu huo na kuwafikisha Mahakamani kwa mujibu wa sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *