Idara ya Uhamiaji ya Nchini, imethibitisha kuwapa uraia wachezaji watatu wa timu ya soka ya Singida Black Stars, baada ya wachezaji hao kuomba uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya sheria ya uraia ya Tanzania, Sura ya 357.
Taarifa ya iliyotolewa hii leo Januari 23, 2025 na Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, SSI Paul Msele imeeleza kuwa Wachezaji hao ni Emmanuel Kwame Keyekeh wa Ghana), Josephat Arhur Bada Ivory Coast na Muhamed Damaro Camara wa Guinea.
