Watanzania wawili watekwa na Hamas

Serikali ya Israel imesema watanzania wawili na raia mmoja wa Kusini ni miongoni mwa mateka 224 wanaoshikiliwa na Hamas baada ya mashambulizi ya Oktoba 7 nchini humo.

Balozi wa Tanzania nchini Israel Alex Kallua ameiambia BBC kuwa ofisi yake pia imepata uthibitisho kutoka kwa mamlaka za Israel kuwa raia wawili wa Tanzania ni mateka wa Hamas bila kutaja majina ya wawili hao.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema “Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka mbalimbali nchini Israel inaendelea na juhudi za kuwapata Vijana hao ili kuwaleta katika mazingira salama, Familia za Vijana hao zimejulishwa kuhusu jitihada hizo na Serikali inaendelea kuwasiliana nao”

“Watanzania tisa wanaoishi nchini Israel waliitikia wito wa mpango wa Serikali wa kuwarejesha nyumbani na walipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, tarehe 18 Oktoba 2023”

Wageni kutoka nchi 25 wanazuiliwa na Hamas, ambapo Walichukuliwa wakati wanamgambo kutoka Hamas walipovuka hadi Israel kutoka Gaza na kuua takriban watu 1,400.

Israel tangu wakati huo imelipiza kisasi kwa mashambulizi ya anga huko Gaza, ambayo wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas inasema yameua takriban watu 6,500.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *