Watanzania wawili hawajulikani walipo

Ubalozi wa Tanzania nchini Israel umesema hauna mawasiliano na raia wawili wa Tanzania ambao wanakaa eneo la kusini ambalo limeshuhudia mapambano baina ya wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na jeshi la Israeli.

Balozi wa Tanzania nchini Israel, Alex Kallua amesema mpaka leo asubuhi, ubalozi huo umekuwa na mawasiliano na watanzania takribani 350 waliopo nchini humo kasoro wanafunzi hao wawili.

Balozi kallua amesema, wanaendelea kuwafuatilia watanzania wawili ambao ni wanafunzi waliokuwa wanafanya mafunzo kwa vitendo kusini mwa nchi hiyo, na kuongeza kuwa zinafanyika jitihada za kuwapata kwanza ili kufahamu walipo na hali zao.

Kallua amesema wanafunzi wengine takribani 260 kati ya watanzania zaidi ya 350 wako salama katika maeneo mbalimbali nchini humo na wamekuwa na mawasiliano na ubalozi na wanaendelea kufuatilia hali ya usalama nchini humo ili kuhakikisha kila mtanzania anakuwa salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *